Mtume akikusanya swalah bila maradhi, mvua wala khofu

Swali: Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya swalah mbili akiwa mkazi bila maradhi, mvua wala matope?

Jibu: Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya swalah bila khofu, mvua wala safari. Wanazuoni wamesema kwamba huenda hilo lilikuwa mwanzoni mwa Uislamu au lilikuwa kwa sababu maalum kama maradhi ya jumla au maradhi ya kuenea kwa watu, kisha jambo hilo likaachwa. Hivyo haijuzu kukusanya swalah isipokuwa kwa sababu kama maradhi au safari. Vivyo hivyo mvua ikiwa inawaletea watu uzito, kuna matope na utelezi katika njia, basi wanaweza kukusanya swalah na hapana vibaya kwa sababu ya udhuru unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/225)
  • Imechapishwa: 16/03/2026