Swali: Mimi ni mswaliji mwenye aleji na ninaudhika kwa harufu za waswaliji wengi. Inajuzu kwangu kubaki na kuswali nyumbani kwangu?

Jibu: Ikiwa haya yanakudhuru na yanakuathiri, baki nyumbani mpaka pale litapoondoka tatizo hili. Ama ikiwa halikudhuru wala halikuathiri, basi kuwa na subira na unaweza kuweka kizuizi kinachozuia harufu kuingia ndani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 07/07/2018