Swali: Je, mtu anatoka katika hesabu ya wale watu elfu sabini ambao wataingia Peponi [pasi na hesabu] kwa uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akijifanyia matabano mwenyewe?

Jibu: Hapana. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni wale ambao hawafanyiwi matabano.”

Bi maana ni yule ambaye anamuomba mwingine amfanyie matabano. Ama kama anajifanyia matabano mwenyewe hakuna neno kwa sababu hakumuomba yeyote amfanyie matabano. Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye mwenyewe alikuwa akijifanyia matabano. Hata hivyo itambulike kuwa kuomba mtu akusomee ni jambo linalofaa. Lakini wale watu elfu sabini hawamuombi yeyote awafanyie matabano. Lengo hawataki wamili kwa mwingine wala hawamuhitajii mwingine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 30/09/2018