Mtu kuitwa ´Abdun-Nabiy na ´Abdul-´Aliy?

Swali: Vipi kuitwa ´Abdun-Nabiy na ´Aliy?

Jibu: Haijuzu kunasibisha kuwa ni mja wa asiyekuwa Allaah. Haijuzu. Haijuzu kuitwa ´Abdul-Ka´bah na ´Abdun-Nabiy kwa maafikiano ya waislamu. Haijuzu kuitwa hivo kwa maafikiano ya waislamu.

Swali: Je, ni lazima abadilishe jina lake?

Jibu: Ndiyo.

Swali: Je, alibadilishe pia ikiwa ni jina la baba yake?

Jibu: Hapana, yaliyopita hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakubadilisha ´Abdul-Muttwalib wala ´Abdul-Manaaf.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24673/تحريم-التسمي-بـ-عبد-النبي-ووجوب-تغييره
  • Imechapishwa: 23/11/2024