Mtu kuendelea kuswali wakati wudhuu´ unapokatika

Swali: Niliingia katika swalah pamoja na imamu na nikakumbuka kuwa nina hadathi. Nyuma yangu kulikuwa safu nyingi, nikahisi ugumu kukata swalah yangu. Kwa hivyo nikawa nimekamilisha swalah pamoja nao mpaka swalah ilipomalizika, kisha nikairudi baada ya kutia wudhuu´. Je, juu yangu kuna kitu kwa kitendo hichi?

Jibu: Ndio. Haijuzu kwako kuswali na wewe hauna twahara. Angalau kwa uchache kaa chini na usiswali pamoja nao na usiwafuate. Katika hali hii unakuwa ni mwenye udhuru ukishindwa kutoka. Lakini kuswali, haijuzu kwako kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-01.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014