Mtu anapata thawabu kwa kuchinja Udhhiyah kinyume na wakati wake?

Swali: Kuna mtu amejikurubisha kwa Allaah kwa kuchinja Udhhiyah lakini katika usiokuwa wakati wa Udhhiyah. Je, anapata ujira?

Jibu: Ni jambo linalojulikana ya kwamba kujikurubisha kwa Allaah katika wakati usiokuwa wa Udhhiyah basi mtu hapati ujira wa Udhhiyah. Lakini hata hivyo akitoa swadaqah nyama yake anapata thawabu za kutoa swadaqah. Ama kusema kwamba anapata thawabu za Udhhiyah sivyo hivyo. Kwa ajili hiyo tunamwambia usijikurubishe kwa Udhhiyah isipokuwa kwa nia ya kwamba unataka kujikurubisha kwa kuitoa ile nyama yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (27/10)
  • Imechapishwa: 19/08/2018