Mtu anafutiwa madhambi baada ya Hajj?

Swali 34: Ikiwa mtu ana madhambi miongoni mwa makubwa, kisha akahiji, je, Allaah humfuta madhambi hayo baada ya kutubu?

Jibu: Ikiwa mtu atatubu kutokana na madhambi – hata kama hakuhiji – na tawbah ikawa ya kweli, basi hakika Allaah (Ta´ala) humfuta yote kabisa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ

“Wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mungu mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah ameiharamisha isipokuwa kwa haki na wala hawazini; atakayefanya hivyo… “

Kwa maana hakumshirikisha Allaah, hakumuua mtu na wala hakuzini:

ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا

“… atakutana na adhabu – ataongezewa adhabu maradufu siku ya Qiyaamah na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika.”[1]

Wewe ikiwa utatubu kwa Allaah tawbah ya kweli – hata kama hutahiji – basi hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hufuta maovu yako.

[1] 25:68-70

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/39)
  • Imechapishwa: 02/06/2026