Hakuna makinzano kati ya wanazuoni ya kwamba Basmalah ni sehemu ya Aayah ndani ya Suurah ”an-Naml”, ilihali Suurah al-Faatihah ina Aayah saba. Basi wale wanazuoni walisoema kuwa Basmalah ni Aayah kutoka ndani ya al-Faatihah wamezingatia Basmalah ndani ya zile saba. Wale walisoema kuwa siyo sehemu ya al-Faatihah wamezingatia Aayah ya saba kuwa ni:
غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ
“… si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”[1]
Miongoni mwa dalili zinazoonyesha ya kwamba Basmalah sio Aayah ndani ya al-Faatihah ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth al-Qudsiy:
“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: ”Nimeigawanya swalah baina Yangu na mja Wangu sehemu mbili na mja Wangu anapata kile anachoomba. Mja anaposema:
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
”Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[2]
Allaah husema:
”Mja Wangu amenisifu…'”
Ameipokea Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah (395). Kwa maana ya kwamba hakutaja Basmalah ndani yake.
[1] 1:6-7
[2] 01:01
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 51
- Imechapishwa: 03/06/2026
Hakuna makinzano kati ya wanazuoni ya kwamba Basmalah ni sehemu ya Aayah ndani ya Suurah ”an-Naml”, ilihali Suurah al-Faatihah ina Aayah saba. Basi wale wanazuoni walisoema kuwa Basmalah ni Aayah kutoka ndani ya al-Faatihah wamezingatia Basmalah ndani ya zile saba. Wale walisoema kuwa siyo sehemu ya al-Faatihah wamezingatia Aayah ya saba kuwa ni:
غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ
“… si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”[1]
Miongoni mwa dalili zinazoonyesha ya kwamba Basmalah sio Aayah ndani ya al-Faatihah ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth al-Qudsiy:
“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: ”Nimeigawanya swalah baina Yangu na mja Wangu sehemu mbili na mja Wangu anapata kile anachoomba. Mja anaposema:
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
”Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”[2]
Allaah husema:
”Mja Wangu amenisifu…'”
Ameipokea Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah (395). Kwa maana ya kwamba hakutaja Basmalah ndani yake.
[1] 1:6-7
[2] 01:01
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 51
Imechapishwa: 03/06/2026
https://firqatunnajia.com/44-dalili-kwamba-basmalah-siyo-sehemu-katika-al-faatihah/