45. Sifa zote njema moja kwa moja ni kwa Allaah

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ

”Himdi zote njema ni za Allaah… ”[1]

Hili ni kwa wingi na linakusanya himidi zote.

Kuhusu uzuri ambao mtu hana taathira juu yake, kama mfano wa urembo na mfano wake, kusifiwa kwayo kunaitwa matapo (المدح) na sio himdi.

MAELEZO

Waja kumsifia Mola wao ni ´ibaadah. Ni miongoni mwa Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah ambayo ni kumpwekesha Allaah kwa matendo ya waja Wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye anayestahiki himdi na sifa kwa kila neema anayopata mja, ni mamoja kuna mja miongoni mwa waja aliyesababisha au kinyume chake, kwa kuwa fadhilah zote ni kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Amesema (Ta´ala):

وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ

“Neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika wasia yake kwa Ibn ´Abbaas:

“Tambua ya kwamba ya kwamba ummah mzima wakikusanyika ili kukunufaisha  basi hawatokunufaisha isipokuwa kwa kitu ambacho Allaah ameshakuandikia.”

Kwa hiyo sifa zote kwa hakika ni za Allaah pekee. Yeye peke Yake ndiye Mwenye kustahiki kusifiwa katika kila hali. Kuhusu waja, basi yale mazuri wanayoyafanya kwa khiyari yao wenyewe – kama vile ihsani na kufanya mema – wanasifiwa kwayo. Yale mazuri yanayopatikana kwao pasi na wao kutokuwa na mchango wowote – kama vile uzuri wa sura na tabia njema – wanatapwa lakini hawasifiwi.

[1] 01:02

[2] 16:53

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 03/06/2026