Swali: Mtu anadai kuwa amekutana na jini ambapo wakafanya ahadi ya kushirikiana katika kheri na nasaha. Jini akamfundisha maneno ya kumuita. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Sijui katika hili kitu cha kukataza moja kwa moja, kwa sababu majini wanaweza kujitokeza, kuonekana kwa baadhi ya watu na wanaweza kuzungumza. Wametusimulia baadhi ya watu waaminifu kuwa wamewasikia majini wakihudhuria vikao vya elimu, wakiridhia haki na kuongoka. Ikiwa jini huyo ameonyesha kheri na akafanya ahadi ya kuitikia mwito wa Allaah, kutubu, kumpwekesha Allaah na kuwafundisha watu wake, basi hatuoni ubaya katika hilo. Lakini kumtumia jini katika mambo ya watu au kumuomba katika ghaibu, hilo halijuzu. Ama kuzungumza naye kwa kheri na kumpa nasaha, hakuna ubaya. Ikiwa mtu anaweza kuzungumza naye, akamnasihi, akamwambia amche Allaah, awafundishe watu wake na kumwelekeza katika kheri, basi hilo halina ubaya.
Wametueleza baadhi ya watu waaminifu kuwa jini walikuwa wanahudhuria vikao vya elimu na mmoja wao alisema kuwa amenufaika na akaongoka, kisha akaaga kwa sababu anaenda katika jihaad pamoja na kundi lake na akakhofia kufa. Mambo kama haya hutokea kwa baadhi ya watu.
Kwa hiyo kumpa nasaha na kumuelekeza katika kheri, basi hapana vibaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3225/روية-الجن-وسماعهم
- Imechapishwa: 18/10/2026
Swali: Mtu anadai kuwa amekutana na jini ambapo wakafanya ahadi ya kushirikiana katika kheri na nasaha. Jini akamfundisha maneno ya kumuita. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Sijui katika hili kitu cha kukataza moja kwa moja, kwa sababu majini wanaweza kujitokeza, kuonekana kwa baadhi ya watu na wanaweza kuzungumza. Wametusimulia baadhi ya watu waaminifu kuwa wamewasikia majini wakihudhuria vikao vya elimu, wakiridhia haki na kuongoka. Ikiwa jini huyo ameonyesha kheri na akafanya ahadi ya kuitikia mwito wa Allaah, kutubu, kumpwekesha Allaah na kuwafundisha watu wake, basi hatuoni ubaya katika hilo. Lakini kumtumia jini katika mambo ya watu au kumuomba katika ghaibu, hilo halijuzu. Ama kuzungumza naye kwa kheri na kumpa nasaha, hakuna ubaya. Ikiwa mtu anaweza kuzungumza naye, akamnasihi, akamwambia amche Allaah, awafundishe watu wake na kumwelekeza katika kheri, basi hilo halina ubaya.
Wametueleza baadhi ya watu waaminifu kuwa jini walikuwa wanahudhuria vikao vya elimu na mmoja wao alisema kuwa amenufaika na akaongoka, kisha akaaga kwa sababu anaenda katika jihaad pamoja na kundi lake na akakhofia kufa. Mambo kama haya hutokea kwa baadhi ya watu.
Kwa hiyo kumpa nasaha na kumuelekeza katika kheri, basi hapana vibaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3225/روية-الجن-وسماعهم
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/mtu-anadai-kuwa-amekutana-na-jini/