Swali: Watu wana imani kama iliyotajwa, tumewabainishia haki lakini hawajakubali. Je, inajuzu kukaa nao? Wakifa, je, waombewe msamaha? Wakifa katika ujinga, je, waombewe du´aa pia?
Jibu: Juu yako ni kubainisha tu. Muumini, mwanachuoni na mwanafunzi anawajibika kubainisha, kulingania kwa Allaah, kuongoza na kuelekeza. Ama kukubali kwa anayeitwa, kuridhia na kuongoka, hilo liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ
”Si juu yako kuwaongoza, lakini Allaah anamwongoza amtakaye.”[1]
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ
”Hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye.”[2]
Anaambiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa hiyo walinganiaji jukumu lao ni kufikisha, kubainisha na kutoa nasaha na Allaah ndiye humwongoza amtakaye. Ikiwa umewaita katika kheri, katika Tawhiyd, imani na Sunnah na kuacha Bid´ah, lakini hawakuitikia basi wakate na usiwe rafiki yao, wahame, usiwaalike nyumbani kwako na wala usikubali mwaliko wao mpaka waache batili waliyonayo. Kwa sababu ukiwa rafiki yao, ukawaalika au ukaitikia mwaliko wao inaonyesha kuridhia matendo yao. Hivyo usiridhie matendo yao, lakini endelea na nasaha, ulingano, uelekezo na unaweza kumtuma mtu unayemwona ana uwezo awaendee ili awalinganie kwa Allaah. Huenda kwa kufanya hivo wakaitikia.
[1] 02:272
[2] 28:56
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3224/حكم-مجالسة-اهل-البدع-ومخالطتهم
- Imechapishwa: 18/10/2026
Swali: Watu wana imani kama iliyotajwa, tumewabainishia haki lakini hawajakubali. Je, inajuzu kukaa nao? Wakifa, je, waombewe msamaha? Wakifa katika ujinga, je, waombewe du´aa pia?
Jibu: Juu yako ni kubainisha tu. Muumini, mwanachuoni na mwanafunzi anawajibika kubainisha, kulingania kwa Allaah, kuongoza na kuelekeza. Ama kukubali kwa anayeitwa, kuridhia na kuongoka, hilo liko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ
”Si juu yako kuwaongoza, lakini Allaah anamwongoza amtakaye.”[1]
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ
”Hakika wewe huwezi kumwongoza umpendaye.”[2]
Anaambiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa hiyo walinganiaji jukumu lao ni kufikisha, kubainisha na kutoa nasaha na Allaah ndiye humwongoza amtakaye. Ikiwa umewaita katika kheri, katika Tawhiyd, imani na Sunnah na kuacha Bid´ah, lakini hawakuitikia basi wakate na usiwe rafiki yao, wahame, usiwaalike nyumbani kwako na wala usikubali mwaliko wao mpaka waache batili waliyonayo. Kwa sababu ukiwa rafiki yao, ukawaalika au ukaitikia mwaliko wao inaonyesha kuridhia matendo yao. Hivyo usiridhie matendo yao, lakini endelea na nasaha, ulingano, uelekezo na unaweza kumtuma mtu unayemwona ana uwezo awaendee ili awalinganie kwa Allaah. Huenda kwa kufanya hivo wakaitikia.
[1] 02:272
[2] 28:56
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3224/حكم-مجالسة-اهل-البدع-ومخالطتهم
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/baada-ya-kuwalingania-ahl-ul-bidah-na-wasiitikie/