Msichana wa miaka tisa haiozeshwi isipokuwa kwa idhini yake

Swali: Baba yangu anataka kumwozesha mmoja wa dada zangu kwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tatu bila ridhaa yake. Mtoto huyo hana msimamo wa dini. Tayari alimuozesha dada yangu mkubwa bila ridhaa yake ambapo akaachika. Aidha akamuozesha mwingine bila ridhaa yake ambapo pia akaachwa. Je, inajuzu kumpinga na kukataa ndoa hii?

Jibu: Ni wajibu kwa baba yako – Allaah amuongoze – asimuozeshe msichana isipokuwa kwa idhini yake. Ikiwa msichana amefikisha miaka isiyopungua tisa, hairuhusiwi kumuozesha isipokuwa kwa idhini yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke aliyeachika haolewi mpaka aombwe ruhusa na bikira haolewi mpaka aombwe idhini.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Yeye huona haya.” Akasema: “Idhini yake ni kule kunyamaza kwake.”

Imekuja katika tamko jengine:

”Bikira huombwa idhini na baba yake na idhini yake ni kule kunyamaza kwake.”

Kwa hiyo ni wajibu kwa baba kumuomba idhini yake. Ikiwa amenyamaza inatosha na si lazima aitikie “ndiyo”. Lakini kumlazimisha na kumuoza hali ya kuwa anakataa, hilo halijuzu kwa mujijbu wa maoni sahihi ya wanazuoni. Kuna wanaosema kuwa baba ana haki ya kumlazimisha msichana bikira, lakini haya ni maoni dhaifu na yanapingana na Hadiyth Swahiyh.

Sahihi ni kwamba hamlazimishi ikiwa ana umri wa kuombwa idhini (miaka isiyopungua tisa). Haijuzu kumuozesha akiwa chini ya miaka tisa isipokuwa kwa maslahi ya dini anayoyaona, kama akija mchumba mwema katika dini na elimu ambapo akaogopa kupotea kwake, basi anaweza kumuozesha kabla hajafikia umri wa kuombwa idhini, kama alivyofanya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuoza ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa mdogo. Hilo lilikuwa ni manufaa makubwa kwake. Ama akishafikisha miaka tisa, hairuhusiwi kumuozesha isipokuwa kwa idhini yake, sembuse msichana mwenye miaka kumi na mbili, kumi na tatu na kumi na nne. Kwa hiyo haya ndio maoni sahihi.

Wewe, ikiwa baba hatakubali nasaha yako, basi peleka jambo hilo mahakamani na mahakama itaangalia suala hilo. Ama wewe usimwambie baba yako isipokuwa maneno mazuri; kuwa na adabu, mpe nasaha kwa upole. Ikiwa hatakubali, basi tafuta watu wema miongoni mwa ndugu au majirani wamsaidie kumshauri kwa njia nzuri. Hairuhusiwi kwake kuwadhulumu wasichana zake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3223/حكم-تزويج-البكر-بدون-رضاها
  • Imechapishwa: 18/10/2026