Masimulizi mengine yanayofahamisha yale yaliyotangulia
88 – Khaythamah bin Sulaymaan ametukhabarisha: Abu Yahyaa bin Abiy Maysarah ametuhadithia: ´Abdullaah bin az-Zubayr al-Humaydiy ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia … (ح) ´Abdullaah bin Ibraahiym ametukhabarisha: Ahmad bin al-Furaat ar-Raaziy ametuhadithia … (ح) ´Aliy bin al-´Abbaas al-Ghazziy ametukhabarisha: Muhammad bin Hammaad ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuzindua, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesema:
”Wakati kulipoteremka Aayah:
قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ
“Sema: “Yeye ni muweza wa kukutumieni adhabu kutoka juu yenu.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:
”Najilinda na uso Wako.”,
na:
أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ
“… au kutoka chini ya miguu yenu… ”,
akasema:
”Najilinda na uso Wako.”,
na:
أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ
“… au akutatanisheni mfarikiane kuwa makundimakundi na akuonjesheni baadhi yenu nguvu za wengineo.”
akasema: ”Haya ni mepesi.”[2]
89 – Ahmad bin al-Hasan na ´Umar bin Muhammad al-Bazzaar wametukhabarisha: Ahmad bin ´Umar bin Abiy ´Aaswim ametuhadithia: Ahmad bin ´Ubaydah al-´Aswfariy ametuhadithia: Ya´quub bin Ishaaq ametuhadithia: Sulaymaan bin Mu´aadh ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-ul-Munkadir, kutoka kwa Jaabir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Hakuombwi kwa uso wa Allaah isipokuwa Pepo tu.”[3]
Miongoni mwa Hadiyth zinazohusiana na maudhui hayo ni:
”Yeyote anayekuombeni kwa uso wa Allaah, basi mpeni.”[4]
Miongoni mwazo pia ni:
”Amelaaniwa mwenye kuomba kwa uso wa Allaah.”
Hata hivyo haikuthibiti kwa upande wa wasimulizi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
Hivo ni kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba aliomba kwa uso wa Allaah, akajilinda kwa uso wa Allaah na akamwamrisha mwenye kuomba kwa uso wa Allaah apewe; yote hayo yamesimuliwa kupitia njia zinazotambulika zenye cheni za wapokezi nzuri. Maimamu wameyasimulia kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, Zayd bin Thaabit, Abu Usaamah, ´Abdullaah bin Ja´far na wengineo.
[1] 6:65
[2] al-Bukhaariy (4628).
[3] Abu Daawuud (1671) na an-Nasaa’iy (5/62). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1671).
[4] Abu Daawuud (5109), an-Nasaa’iy (2567) na Ahmad (5365). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (5109).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 97-99
- Imechapishwa: 18/10/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 97-99
Imechapishwa: 18/10/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/40-kuomba-kinga-kwa-uso-wa-allaah/