Masimulizi mengine yanayojulisha kutazama uso wa Allaah

87 – Khaythamah bin Ahmad ametukhabarisha: Muhammad bin ´Awn bin Sufyaan ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muusa ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuzindua, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika du´aa yake:

اللَّهُمَّ إنّي أَسْأَلُكَ الرِّضَا بَعْدَ الْقَضَاءِ وَأَسْأَلُكَ بَرْدَ الْعَيْشِ بعد الْمَوتِ وَأَسْأَلكَ لَذَّةَ النَّظرِ إِلى وَجْهِكَ والشَّوْقَ إِلى لِقَائِكَ في غيرِ ضَرَّاءَ مُضِرَّةٍ وَلاَ فِتْنَةٍ مُضِلَّةٍ اللَّهُمَّ زَيِّنَّا بِزِينةِ الإِيْمانِ وَاجْعَلْنَا هُدَاةً مُهْتَدِينَ

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba radhi baada ya hukumu. Nakuomba maisha mazuri baada ya kufa. Nakuomba ladha ya kuutazama uso Wako. Nakuomba kutamani kukutana Nawe bila ya madhara wala mtihani zinazopotosha. Ee Allaah! Tupambe kwa pambo la imani na Utujaalie kuwa waongofu wenye kuongoza.”[1]

Hammaad bin Salamah amepokea mfano wake kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib. Ameipokea vilevile Abud-Dardaa’, kutoka kwa Zayd bin Thaabit, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] an-Nasaa’iy (1305) na Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan (509 – al-Mawaarid) na al-Albaaniy katika ”as-Sunnah” (424).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 97
  • Imechapishwa: 18/10/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy