Masimulizi mengine yanayofahamisha kutazama uso wa Allaah

83 – ´Abdur-Rahmaan bin Yahyaa na ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Muqriy wametukhabarisha: Abu Mas´uud Ahmad bin al-Furaat ametuhadithia: Abu Daawuud ametuzindua: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Swuhayb, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.”[1]

”Kutazama uso wa Mola wao (Jall wa ´Azz).”[2]

Ibn Mas´uud pia amesema:

”Kutazama uso wa Mola (Jall wa ´Azz).”

84 – al-Hasan bin Yuusuf at-Twaraa-ifiy na Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm wametukhabarisha huko Misri na huko Neyshabur: Ibraahiym bin Marzuuq ametuhadithia: ´Uthmaan bin ´Umar ametuhadithia: Israa’iyl ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa ´Aamir bin Sa´d, ambaye ameeleza kuwa Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.”

”Kutazama uso wa Allaah (Jall wa ´Azz).”

Hivo pia ndivo alivyofasiri Aayah hiyo Hudhayfah bin al-Yamaan.

85 – Ismaa´iyl bin Muhammad as-Swaffaar ametukhabarisha huko Baghdaad: al-Hasan bin ´Arafah ametuhadithia: Silm bin Saalim ametuhadithia, kutoka kwa Nuuh bin Abiy Maryam, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu Aayah hii:

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata Pepo na zaidi.”

Akajibu: ”Wale waliofanya matendo mazuri duniani watapata Pepo – na ziada, ni kutazama uso mtukufu wa Allaah (Jalla wa ´Azz).”

[1] 10:26

[2] Ahmad (4/332), Muslim (181) na at-Tirmidhiy (2558).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 18/10/2026
  • Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy