Swali: Nimeibiwa kiasi kikubwa cha pesa na tangu hapo nimejaa huzuni na msongo wa mawazo ulioathiri afya yangu. Unanishauri nini?
Jibu: Tunakuusia umnyenyekee Allaah, uondoe katika moyo wako maumivu haya na umwombe akulipe badala ya yaliyopotea. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ
“Hausibu msiba wowote [kukupateni] isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Yeyote anayemuamini Allaah, basi huuongoza moyo wake.”[1]
Kwa maana isipokuwa kwa mipango na makadirio ya Allaah.
وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ
”Yeyote anayemuamini Allaah, basi huuongoza moyo wake.”
Baadhi ya Salaf wamesema:
”Ni mtu anayepatwa na msiba ambapo akajua kuwa umetoka kwa Allaah na hivyo anaridhia na anasalimu amri.
Kwa hiyo ni juu yako kuhisi kuwa hili limetokea kwa ujuzi wa Allaah na kwa makadirio Yake. Matokeo yake ridhia hilo na umwombe akurudishie ulichopoteza au akulipe kilicho bora zaidi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ
”Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu kidogo katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [ya kazi zenu]. Wabashirie wenye kusubiri.”[2]
Wewe umejaribiwa kwa kupungua mali kwa kuibiwa na Allaah amesema:
وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ
“Wabashirie wenye kusubiri – wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”[3]
Ukipata haya – rehema, baraka na uongofu – basi bishiria mwisho mwema na malipo bora kutoka kwa Mola wako. Usijali sana kilichoibiwa. Hilo limekwishatangulia katika ujuzi na makadirio ya Allaah. Kwa hiyo ni juu yako kusubiri mpaka upate mbadala ulio bora zaidi na kurejea kwa Allaah na kumuomba katika fadhilah Zaxke. Usihuzunike; jambo hili ni jepesi.
[1] 64:11
[2] 02:155
[3] 02:155-157
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3227/الصبر-عند-المصاىب
- Imechapishwa: 18/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3227/الصبر-عند-المصاىب
Imechapishwa: 18/10/2026
https://firqatunnajia.com/amepatwa-na-huzuni-na-msongo-mkubwa-wa-mawazo-baada-ya-kuibiwa-pesa/