Mtu amtaje Allaah vipi wakati wa kutawadha akiwa chooni?

Swali: Mtu akiwa chooni ataleta Tasmiyah vipi?

Jibu: Mtu akiwa chooni basi amtaje Allaah kwa moyo na si mdomo wake. Kwa sababu uwajibu wa kumtaja Allaah kabla ya kutawadha na kuoga sio kwa maneno. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna kitu kisilichosihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Tasmiyah wakati wa wudhuu´.”

Hayo ndio maoni vilevile ya Muwaffaq, ambaye ni mwandishi wa “al-Mughniy” na wengineo ya kwamba kumtaja Allaah kabla ya kutawadha ni Sunnah na sio wajibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/110)
  • Imechapishwa: 14/06/2017