Mtu aliyepoteza kiungo kinachotakiwa kuoshwa anatawadha vipi?

Swali: Ambaye amepoteza kiungo cha mwili atatawadha vipi? Je, akiwekwa kiungo cha bandia akioshe?

Jibu: Mtu akipoteza kiungo chake cha mwili miongoni mwa vile viungo vinavyotiwa wudhuu´, basi ule uwajibu wake wa kukiosha unaanguka mbali na Tayammum. Kwa sababu amepoteza pahali pa faradhi na hivyo hakuna kinachomuwajibikia. Hata kama atapandikiziwa kiungo cha bandia haimlazimu kukiosha. Haitakiwi kusemwa kwamba kiungo hichi ni kama soksi ambayo inatakiwa kupanguswa. Soksi amezivaa juu kiungo kilichopo ambacho ni wajibu kwake kukiosha. Ama kiungo hichi feki kimepandikizwa juu ya kitu kisichokuwepo. Lakini wanachuoni wanasema kiungo hicho kikikatwa kuanzia msingi wake, basi itakuwa ni wajibu kuosha kile kilele cha kiungo. Kwa mfano lau mkono utakatwa kuanzia mwanzo wake, basi itakuwa ni wajibu kuosha kile kilele cha kiungo hicho. Iwapo mguu utakatwa kuanzia fundo mbili za miguu, basi itakuwa ni wajibu kuosha ncha ya muundi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/152)
  • Imechapishwa: 01/07/2017