Kuhusiana na msemo wa baadhi ya watu wapumbavu wanaosema kuwa sio wajibu kwa wananchi kumtii mtawala mpaka wawe wamenyooka kikamilifu, hili ni kosa. Hili halina lolote kuhusiana na Shari´ah. Bali haya ni madhehebu ya Khawaarij. Khawaarij wanataka mtawala awe ni mwenye kufuata maamrisho ya Allaah katika kila kitu. Hili halipatikani tokea huko kale tangu mambo yalipobadilika.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/425)
  • Imechapishwa: 11/08/2025