Mswaliji mmoja ametoka katika safu kumwacha mwenzie akiwa peke yake

Swali: Ikiwa watu wawili wanaswali katika safu ambapo mmoja wao akatoka katika safu na akabakia mmoja?

Jibu: Asogee mbele upande wa kuliani mwa imamu.

Swali: Ni wawili wanaoswali – Allaah akubariki – wanaoswali nyuma ya safu ambapo mmoja wao akatoka katika safu kwa ajili ya kukidhi haja yake na akabakia yule mwingine peke yake akiswali nyuma ya safu?

Jibu: Dhahiri ni kwamba atatafuta [mwenzie].

Swali: Ameshaleta Takbiyr na kuingia ndani ya safu?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23794/ما-حكم-اثنين-يصليان-بالصف-فخرج-احدهما
  • Imechapishwa: 04/05/2024