Mswaliji anayejiunga na anayeswali peke yake nyuma ya safu na kumvuta aliyeko mbele ya safu aswali nawe

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ambaye anaswali peke yake  nyuma ya safu lakini akaja mwingine na kuswali naye?

Jibu: Ikiwa amejiunga naye katika Rak´ah ya kwanza basi inasihi swalah zao wote wawili. Na ikiwa wameshaswali Rak´ah moja basi aikate na kuianza swalah yake kuanzia pale ambapo alikuja mtu mwingine kujiunga naye ili swalah yake isihi.

Swali: Inasihi ile Takbiyrat-ul-Ihraam?

Jibu: Ndio, inasihi mpaka atakaporukuu. Akisharukuu na asije yeyote inabatilika, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikubali Rak´ah ya Abiy Bakrah aliyojiunga nje ya safu kisha baadaye ndio akajiunga na safu.

Swali: Je, inafaa kwa mtu anayeswali peke yake nyuma ya safu kumvuta mswaliji aliyeko safu ya mbele?

Jibu: Haifai kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23796/حكم-من-صلى-منفردا-ثم-اتى-شخص-معه
  • Imechapishwa: 04/05/2024