Swali: Imamu anapotoa salamu upande wa kulia wakamfuata maamuma, kisha akatoa salamu upande wa kushoto wakamfuata?
Jibu: Huyu anauliza kuhusu ikiwa maamuma wanatoa salamu pamoja na imamu; baada ya salamu ya kwanza wanatoa ya kwanza, na baada ya ya pili wanatoa ya pili. Jibu ni kwamba hakuna tatioz, ni sahihi na haidhuru. Lakini Sunnah, aula na bora zaidi ni wao wachelewe hadi atoe salamu ya pili na wasiwe na haraka. Anapotoa salamu ya kwanza, wao wasitoe salamu mpaka atoe ya pili. Hivi ndio dhahiri ya Hadiyth na kwa kukamilisha kumfuata imamu. Lakini akitoa salamu baada ya kwanza wakatoa ya kwanza, na baada ya ya pili wakatoa ya pili, swalah yake inasihi na halina tatizo wala dhambi. Hata hivyo ameacha lililo bora, lililo kamili na lililo salama zaidi. Kilichopasa ni wawe watulivu na wasiharakishe mpaka imamu atapotoa salamu ya pili. Akitoa ya pili, ndipo wao watoe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Anapoleta Takbiyr, nanyi leteni Takbiyr, anaporukuu, nanyi rukuuni.”
Kwa hiyo msirukuu mpaka yeye arukuu kwanza. Wachelewe mpaka atoe salamu ya pili, hili ndilo salama zaidi na lililo kamili katika kumfuata. Akitoa salamu ya kwanza baada ya ya kwanza, na ya pili baada ya ya pili, tunataraji hakuna neno. Hata hivyo ameacha lililo salama na bora zaidi.
Swali: Kuna Hadiyth katika ”as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy yenye maana ya kuonyesha kwamba akitoa salamu kulia baada ya imamu baada ya salamu ya kwanza moja kwa moja huenda hiyo salamu inatosha na akichenguka wudhuu´ baada yake basi swalah yake inakuwa sahihi?
Jibu: Kuna mitazamo tofauti kati ya wanazuoni juu ya hilo. Wengi wanasema salamu ya kwanza inatosha. Akitoa ya kwanza inatosha. Akichengukwa na wudhuu´ baada yake, basi swalah yake inasihi. Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa ni lazima salamu mbili. Kwa sababu haifungwi swalah na wala haimaliziki isipokuwa kwa salamu ya pili. Kwa mujibu wa maoni haya akichenguka wudhuu´ baina ya salamu mbili, basi swalah inabatilika na hivyo ni lazima airudie. Hili ndilo lenye nguvu. Lenye nguvu ni kwamba lazima ziwe salamu mbili. Kwa hiyo inampasa asiwe na haraka. Kundi la wengi wao wanaona kwamba akitoa ya kwanza inatosha, ya pili ni Sunnah na si wajibu kwao. Wanaona kuwa ya kwanza inatosha. Lakini lenye nguvu na bora kwa mujibu wa dalili ni kwamba zote mbili ni wajibu na ni katika nguzo za swalah. Kwa hiyo inatakiwa kuzihifadhi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1068/حكم-متابعة-الامام-في-كل-تسليمة
- Imechapishwa: 28/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1068/حكم-متابعة-الامام-في-كل-تسليمة
Imechapishwa: 28/01/2026
https://firqatunnajia.com/mswaliji-anatoa-salamu-ya-kwanza-kabla-ya-imamu-wake-kuleta-salamu-ya-pili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket