Swali: Kuna mtu aliswali na akasahau kuwa yuko na ubani mdomoni mwake ambapo akaitema. Ni upi sahihi wa swalah yake?

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Haina neno. Swalah yake ni sahihi hata kama atabakiza ubani mdomoni. Lakini asile kitu au kunywa kitu na huku anaswali. Lakini kule kuwa na kitu mdomoni haina neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 25/02/2022