Msomaji wa Qur-aan anapanga malipo kabla ya matabano

Swali: Mwanamume anawasomea wagonjwa kwa Qur-aan na du´aa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kabla ya kusoma anabainisha kiasi cha mali atakachochukua kutoka kwa mgonjwa. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hakuna ubaya katika hilo ikiwa anasoma yale yaliyo rahisi katika Qur-aan, anawaombea du´aa na anampulizia mgonjwa, hakuna ubaya kubainisha ujira wake. Kama ilivyotokea kwa baadhi ya Maswahabah pamoja na mwenye kuumwa aliyeng’atwa. Walikuwa wamewashukia watu hao nao hawakuwakarimu. Kisha wakaja kwao wakiomba mtu wa kumsomea mgonjwa huyo, wakasema: ”Isipokuwa mtupangie sehemu ya ujira.” Wakawapangia sehemu fulani ya kundi la kondoo. Wakamtabana hadi Allaah akamponya na hivyo wakawakabidhi ujira wao. Wakaenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye akawakubalia juu ya jambo hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1362/حكم-اخذ-المال-مقابل-الرقى-الشرعية-على-المرضى
  • Imechapishwa: 14/12/2025