Msingi ni kwamba waislamu wote wanaswaliwa

Swali: Akiwa na shaka juu ya jeneza kama ni la mtu Sunniy, Raafidhwiy au mwengine. Je, aweke sharti?

Jibu: Muda wa kuwa ni miongoni mwa waislamu, basi ataswaliwa na himdi zote njema anastahiki Allaah – isipokuwa ikiwa atajua wazi kwamba mtu huyo ni miongoni mwa wasiofaa kuswaliwa au ikiwa atajua kuwa ni kafiri.

Swali: Lakini Ibn-ul-Qayyim amenukuu jambo hilo kutoka kwa Shaykh-ul-Islaam?

Jibu: Kuweka sharti ni jambo hakuna dalili juu yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27526/هل-يجوز-الاشتراط-لمن-شك-في-اعتقاد-الميت
  • Imechapishwa: 11/04/2025