Msingi kwa mwanaume ni kuwa na kuoa wake wengi

Swali: Je, msingi katika ndoa ni kuwa na mke mmoja na kuoa wake wengi kumekuja kwa hali ya dharurah kwa sababu fulani au ni kinyume chake?

Jibu: Msingi ni kuoa wake wengi na mke mmoja hupatikana pale panapokuwepo udhaifu au kushindwa. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Ala) amesema:

وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi [bakieni na] mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.”[1]

Hii inaonesha kwamba msingi ni kuoa wake wengi; anaoa wawili, watatu au wanne. Kwa sababu hilo ni karibu zaidi na kumlinda mwanaume na uzinzi na ni karibu zaidi na kuongezeka kwa kizazi. Kwa hiyo akishindwa na akakhofia kutokuwa na uadilif, basi  atosheke na mke mmoja, pamoja na waliomrahisikia miongoni mwa wajakazi.

[1] 04:03

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1782/هل-الاصل-في-الزواج-التعدد
  • Imechapishwa: 27/12/2025