Msimamo wa mke kwa ami yake mume na watoto wa kaka yake

Swali: Ni ipi hukumu ya mke wa ami kujifunua mbele ya mtoto wa kaka yake mume hata kama kiumri wanatofautiana kiasi kikubwa?

Jibu: Haifai kwa mwanamke kujifunua mbele ya kaka yake mume wake, ami yake mume wake, mabinamu zake mume wake wala watoto wa kaka yake mume wake. Wote hawa ni watu ajinabi kwake. Inafaa tu kujifunua mbele ya mume wake, baba yake, babu yake au watoto wake.

Ama kuhusu kaka, baba wakubwa na baba wadogo, wajomba na watoto wa kaka yake wote hawa ni ajinabi kwa mwanamke. Haijuzu kwake kujifunua mbele yao wala kukaa nao chemba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12295/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%83%D8%B4%D9%81-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D9%88%D8%AC%D9%87%D9%87%D8%A7-%D9%84%D8%A7%D9%82%D8%A7%D8%B1%D8%A8-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 17/07/2020