Ibaadhiyyah wanaonelea kufaa kuuawa kila yule anayekosoa madhehebu yao

Vilevile Ibaadhiyyah wanahukumu kumuua kila yule ambaye anakosoa kwa wazi masuala yoyote kutoka katika dini ya Ibaadhiyyah katika yale mambo ambayo Ummah umetofautiana kwayo. Bali hata kama hakukosoa kwa uwazi bali alichofanya tu ni kuashiria hilo. Hukumu yake ni kuuawa. Wanaonelea kuwa kiongozi ambaye ni shabiki wa dini ya Ibaadhiyyah ndiye anatakiwa kumsimamishia adhabu hiyo ya kumuua. Endapo hawatokuwa na kiongozi basi itajuzu kumuua mpinzaji mauaji ya kuvizia. Huu ni uwekaji Shari´ah na kusapoti mwenendo wa mauaji na kuwasafisha wapinzani kwa siri kwa sababu tu ya madhehebu.

  • Mhusika: Abuu Swaalih Mustwafaa ash-Sharqaawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kuntu ibaadhwiyyaa yaa layta qawmiy ya´lamuun, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 11/06/2017