Swali: Ni upi wajibu wa muislamu pale ambapo fitina na vurugu inakuwa nyingi na baadhi wanaita katika kumfanyia mtawala uasi na wanaita kuwa ni “Jihaad”?
Jibu: Ni juu yako kuwa na uthabiti katika ´Aqiydah sahihi. Ni juu yako kujitenga mbali na walinganizi hawa; usisuhubiane nao na wala usichanganyike nao. Usiwasikilize wao, kanda zao wala maneno yao. Wanaita katika kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kumuasi mtawala muumini ni kum
uasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule anayemtii kiongozi basi amenitii mimi na yule mwenye kumuasi kiongozi basi ameniasi mimi.”
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
- Imechapishwa: 09/06/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)