Msimamo mkali – tuhumu za wazushi dhidi ya Ahl-us-Sunnah

Swali: Baadhi wanawatuhumu Ahl-us-Sunnah kwamba wana msimamo mkali. Tunawaraddi vipi?

Jibu: Ukweli ni kwamba sisi tunajijua wenyewe zaidi kuliko wengine. Wale wanaotutuhumu kuwa tuna mapungufu na kuchukua wepesi, namshuhudisha Allaah ya kwamba ni wakweli. Vinginevyo sisi tunapenda kuwa wakati na kati; tusiwe wenye kufanya upungufu wala msimamo mkali. Tuko wapi sisi na jambo la kuamrisha mema na kukataza maovu? Tuko wapi sisi na kuwatanguliza wengine yetu? Tuko wapi sisi na jambo la kupupia elimu? Sisi ni wenye kufanya mapungufu. Tunamuomba Allaah atughufurie na atusamehe. Hata hivyo wazushi ni wenye kujigonga kuhusu Ahl-us-Sunnah. Mara husema kuwa wana msimamo mkali, mara nyingine wanasema kuwa wamekaa katika misikiti yao na kazi ni kusomeshana Hadiyth na wameacha kulingania kwa Allaah na kwamba wameacha kupambana jihaad katika njia ya Allaah. Wazushi ni wenye kujigonga juu ya Ahl-us-Sunnah.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 326-327
  • Imechapishwa: 30/04/2025