Wa kwanza: Ambaye hajui upindaji na upotevu alionao. Huyu aelezwe ikiwa lengo lake anaitafuta haki. Aelezwe kwa njia iliokuwa nzuri. Pengine kwa kufanya hivo akarejea – Allaah akitaka.
Wa pili: Mtu ambaye anajua majanga, upindaji na upotevu alionao. Huyu ana hukumu moja na ni kama yeye.
Hakika tumezungumza juu ya mwanaume huyu na kumraddi tangu hapo kale mpaka sasa. Laiti mambo yote ambayo ametumbukiaemo mtu huyu yatakusanywa sehemu moja na mtu akafanya moja katika mambo hayo, basi ingelitosheleza kufanyiwa Tabdiy´. Tusemeje na amekusanya mambo yote hayo! Baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo:
Mosi: Madai na uongo wake juu ya cheo cha utume na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakosea katika njia za Da´wah[1]. Anamtuhumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa janga hili.
Pili: Aliidhinisha kuenezwe kitabu ambapo ndani yake kulikuwa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno yake hayakubaliwi isipokuwa kwa dalili[2]. Ee mfedheheshwaji! Ni dalili ipi unayotaka kwa kumuomba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alete dalili? Je, wewe huzungumzi kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah? Hii ni Sunnah sampuli gani? Hii ni Sunnah ya nani? Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakusema:
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ
“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho.”? (33:21)
al-Hasan al-Baswriy amesema:
“Hapa ni pindi walikuwa wanasema kuwa wao wanampenda Allaah. Ndipo Allaah akataka kuweka alama yenye kuonyesha kweli kumpenda kwa kuteremsha:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu.”” (03:31) Ibn Abiy Haatim katika “az-Zuhd”
Halafu huyu – Yahyaa al-Hajuuriy – anasema kuwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanahitajia dalili.
Tatu: Mtu wa kwanza kutamka kwa Irjaa´ ni ´Uthmaan bin Madh´uun (Radhiya Allaahu ´anh).
Nne: Kuna Maswahabah walioshiriki katika kumuua ´Uthmaan. Ana majanga na mambo mengi tu.
[1] Tazama 886
[2] Tazama 442
- Mhusika: Shaykh ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Bukhaariy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/Rodod/14AqwalOlamaaFiya7yaAl7ajori.mp3
- Imechapishwa: 17/01/2017
Swali: Ni zepi nasaha zako kuhusu Yahyaa al-Hajuuriy? Huku Uingereza kuna vijana wanaomtetea na kumfuata.
Jibu: Tulizungumzia masuala haya tangu hapo kitambo. Hakuna anayemtetea mtu huyu isipokuwa mmoja katika watu wawili:
Wa kwanza: Ambaye hajui upindaji na upotevu alionao. Huyu aelezwe ikiwa lengo lake anaitafuta haki. Aelezwe kwa njia iliokuwa nzuri. Pengine kwa kufanya hivo akarejea – Allaah akitaka.
Wa pili: Mtu ambaye anajua majanga, upindaji na upotevu alionao. Huyu ana hukumu moja na ni kama yeye.
Hakika tumezungumza juu ya mwanaume huyu na kumraddi tangu hapo kale mpaka sasa. Laiti mambo yote ambayo ametumbukiaemo mtu huyu yatakusanywa sehemu moja na mtu akafanya moja katika mambo hayo, basi ingelitosheleza kufanyiwa Tabdiy´. Tusemeje na amekusanya mambo yote hayo! Baadhi ya mambo hayo ni yafuatayo:
Mosi: Madai na uongo wake juu ya cheo cha utume na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakosea katika njia za Da´wah[1]. Anamtuhumu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa janga hili.
Pili: Aliidhinisha kuenezwe kitabu ambapo ndani yake kulikuwa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno yake hayakubaliwi isipokuwa kwa dalili[2]. Ee mfedheheshwaji! Ni dalili ipi unayotaka kwa kumuomba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alete dalili? Je, wewe huzungumzi kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah? Hii ni Sunnah sampuli gani? Hii ni Sunnah ya nani? Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakusema:
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ
“Hakika mna kigezo kizuri kwa Mtume wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho.”? (33:21)
al-Hasan al-Baswriy amesema:
“Hapa ni pindi walikuwa wanasema kuwa wao wanampenda Allaah. Ndipo Allaah akataka kuweka alama yenye kuonyesha kweli kumpenda kwa kuteremsha:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu.”” (03:31) Ibn Abiy Haatim katika “az-Zuhd”
Halafu huyu – Yahyaa al-Hajuuriy – anasema kuwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanahitajia dalili.
Tatu: Mtu wa kwanza kutamka kwa Irjaa´ ni ´Uthmaan bin Madh´uun (Radhiya Allaahu ´anh).
Nne: Kuna Maswahabah walioshiriki katika kumuua ´Uthmaan. Ana majanga na mambo mengi tu.
[1] Tazama 886
[2] Tazama 442
Mhusika: Shaykh ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Bukhaariy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/Rodod/14AqwalOlamaaFiya7yaAl7ajori.mp3
Imechapishwa: 17/01/2017
https://firqatunnajia.com/msimamo-kwa-wafuasi-wanaomtetea-yahyaa-al-hajuuriy-uk/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)