Swali: Mtu anakuja shuleni ilihali hakuswali Fajr ingawa yuko katika darasa la sita au la tano. Hii ina maana kwamba amevuka miaka ya baleghe.

Jibu: Tunamwomba Allaah usalama. Mtu huyu yuko chini ya jukumu la familia yake. Wanatakiwa kumfundisha. Aidha mwalimu anapaswa kumfundisha.

Swali: Je, ni wajibu kwa mwalimu kumfukuza?

Jibu: Ni lazima amzindue juu ya kuswali Fajr ndani ya wakati wake ikiwa amefikia umri wa kuweza kupambanua mambo. Hata hivyo hakuna neno ikiwa hajafikia umri wa kuweza kupambanua mambo. Lakini anapaswa kufundishwa akiwa na umri wa miaka saba au zaidi. Ikiwa ana umri wa miaka kumi au zaidi, basi anastahiki kupigwa. Ni wajibu kwa waalimu kumfundisha na kumwongoza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29325/ما-كيفية-النصح-للطلاب-الذين-لا-يصلون-الفجر
  • Imechapishwa: 02/06/2025