Swali: Mimi nimeoa msichana mwenye miaka kumi na nane. Mpaka sasa hajazaa watoto. Tatizo langu mimi na yeye ni kwamba havai Hijaab mbele ya mtu yeyote wa karibu au mbali na yeye, Mahram yake au asiwe Mahram, anajishaua kwa wingi kwa kuonyesha mapambo, mchafu katika mavazi yake na mwili wake. Haogi katikati ya jimaa isipokuwa asubuhi. Siku zote anapenda kutoka nyumbani kwake. Mavazi yake siku zote ni yenye kupasuka. Anapokuja mtu ajinabi nyumbani anamkaribisha kwa kukaa naye bora kuliko anavofanya kwangu. Ninapomuuliza anasema kuwa mimi nina wivu. Ninapozungumza na familia yake wanasema kuwa mimi si mzuri kwa mke wangu. Nimekuwa ni mwenye kudangana. Hajali kuonyesha baadhi ya uzuri wake kama kifua na mgongo. Ni mwenye kuthubutu kwa wingi kwa kuongea, kucheka na kufanya mazaha na mtu yeyote. Siku zote anatembea masafa marefu kutoka nyumbani kwake na anaenda kwenye baadhi ya nyumba akiwa kichwa wazi. Ninapozungumza naye anasema kuwa watamcheka yeye na si mimi na kwamba yeye ndivo alivo. Matokeo yake nimekuwa ni mwenye kumchukia na simtekelezei baadhi ya mahitajio yake. Ningekuwa na uwezo ningeoa mwanamke mwingine na nikamwacha. Wanawake hii leo mahari yao yamekuwa ghali. Unaninasihi nini? Niwaambia familia yake warudishe mahari yake na nimtaliki, nimpige, nimtaliki pasi na kurudisha chochote katika mahari yake na nimebaki pasi na mke au nivumilie na hali ni kama unavoiona? Naomba ufumbuzi.
Jibu: Jambo hili ni tatizo, kama ndugu alivosema. Naona kama mwanaume hana uwezo wa kuoa mwengine basi abaki na mke wake na apupie kiasi na anavoweza juu ya kumtia adabu kwa kumwelekeza, kumpa mawaidha, kumhama na kumpiga. Hivi khaswa pale ambapo anajinyanyua kwake na kumdharau. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا
“Na wale ambao mnachelea uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao. Kwani hakika Allaah daima ni Mwenye yujuu kabisa, Mkubwa kabisa.”[1]
Naona kuwa mtu mwenye busara ambaye amewafikishwa na Allaah anaweza kumaliza tatizo kama hili kwa njia iliokuwa bora. Pamoja na kumwelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kumuomba amtengenezee mke wake. Mtu akitumia sababu hizi mbili; sababu ya Kishari´ah ambayo ni kumuomba Allaah (´Azza wa Jall) na sababu ya kuhisia ambayo Allaah ameiamrisha kumpa mawaidha, kumhama na kumpiga. Lakini kipigo kisichoumiza. Mtu akitumia hekima kwa muqtadha vile Shari´ah imepelekea basi Allaah (Ta´ala) atamtengenezea hali yake. Amesema (Ta´ala):
وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ
“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia njia ya kutokea.”[2]
وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا
“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia wepesi katika jambo lake.”[3]
[1] 04:34
[2] 65:02-03
[3] 65:04
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (14) http://binothaimeen.net/content/6789
- Imechapishwa: 17/02/2021

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (14) http://binothaimeen.net/content/6789
Imechapishwa: 17/02/2021
https://firqatunnajia.com/msimamo-kwa-mke-mwenye-kila-tabia-mbaya/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)