Msimamo katika kikao ambapo wanachuoni wanatukanywa

Swali: Mtu aliyepewa mtihani kuwepo katika kikao ambapo kuna mtu mzima ambaye anawatukana na kuwaponda wanachuoni amkataze na kumbainishia vipi?

Jibu: Amnasihi na kumtajia dalili zinazoharamisha kusengenya, kueneza uvumi na kukiuka heshima za wanachuoni. Amtajie kisa cha yule aliyesema:

“Hatujapatapo kuona watu kama wasomaji wetu hawa.”

Vilevile amtajie namna Allaah alivyowahukumu. Akitubu na kuachana na haya ni sawa. Vinginevyo simama utoke katika kikao hicho na wala usiikae pamoja nao. Jitenge mbali na kikao chao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (02) http://alfawzan.af.org.sa/node/2045
  • Imechapishwa: 13/10/2016