Msikiti uliojengwa chini ya makazi wanakoeshi watu

Swali: Inafaa kuswali kwenye msikiti uliojengwa chini ya makazi ya watu?

Jibu: Haja ikipelekea kuwepo msikiti chini ya jengo hakuna neno. Haja ikipelekea kwa njia ya kwamba wakazi wa hapo hawana msikiti na akajitolea mtu kuwapa ukumbi wa chini na wakaufanya kuwa msikiti, basi hakuna neno.

Ama ikiwa msikiti tayari umeshajengwa basi kusijengwe juu yake majengo ya makazi. Msikiti ukishajengwa basi juu yake kuachwe kwa ajili ya haja za msikiti. Ama ikiwa msikiti ni mpya ulijengwa kutokea mwanzo juu ya makazi na makazi hayo yalitangulia ambapo mwenye nyumba alijitolea ukumbi wa chini, gorofa ya pili au ya tatu basi hakuna ubaya. Allaah amjaze kheri ikiwa ni wenye kuhitajia kitu hicho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/20575/حكم-الصلاة-بمسجد-مبني-تحت-عمارة-سكنية
  • Imechapishwa: 02/04/2021