Swali: Baadhi ya watu wanasema:

“Msifarikishe kati ya waislmu kwa sababu ya mikhalafa yao. Wanajenga hoja kwa msimamo wa Haaruun (´alayhis-Salaam):

إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ

“Hakika mimi niliogopa usije kusema “Umefarikisha kati ya wana wa Israaiyl.”[1]

Je, utumiaji wao wa dalili na maneno yao ni sahihi?

Jibu: Sisi hatutegemei dini za kale. Sisi tunafuata dini ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hafuati dini zilizotangulia. Dini ya Muhammad imezifuta dini nyenginezo.

[1] 20:94

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (103) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-6-3-1441_1.mp3
  • Imechapishwa: 23/01/2021