Swali: Je, inafaa kwa msichana kumpa mama yake zakaah khaswa kwa kuzingatia kwamba mama yake ni fakiri mno licha ya kwamba sijui kama yeye ndiye humpa matumizi?

Jibu: Haifai kuwapa zakaah wazazi wawili, mababu, mabibi, watoto wa kike, watoto wa kiume, watoto wao wa kiume wala watoto wao wa kike. Haifai kabisa kumpa baba na kupanda juu wala mtoto na kushuka chini. Ni mamoja ni wavulana au wasichana. Bali wakiwa na haja ni lazima kwako kuwahudumia. Inafaa kumpa zakaah kaka, dada, wapwa, wababa wakubwa na wajomba wakiwa si wenye kuishi nyumbani kwako na si wewe mwenye kuwapa matumizi. Wakiwa ni wahitaji basi unatakiwa kuanza nao. Bali wao wana haki zaidi kuliko wengine. Kuwapa swadaqah jamaa ni swadaqah na kuunga kizazi. Kujengea juu ya haya msichana huyu ambaye amempa zakaah yake mama yake haitoshelezi na wala haijuzu kwake kufanya hivo. Bali ni lazima kwake kumpa mtumizi mama yake mbali na pesa ya zakaah kama ni mwenye kuhitaji.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 13/06/2021