Msamaha pale ambapo umechukua haki ya kiumbe

Swali: Nini maana ya maneno yake kwamba anatubia kwa Allaah na kwa Mtume Wake?

Jibu: Ikiwa haki ni ya kiumbe basi mtu anatakiwa kutubia kwake kwa maana ya kwamba akaomba udhuru. Naomba udhuru kwa Allaah, Mtume Wake na kwa viumbe Wake. Imekuja katika tamko jengine:

“Natubia kwa Allaah na situbii kwa Muhammad.”

Akasema:

“Umeitambua haki kwa mwenye nayo.”

Swali: Na (الواو) hapa si inakuwa ya ushirika?

Jibu: Hapana. Maana yake ni kwamba natubia kwa Allaah kutokana na haki Yako na natubia kwako kutokana na haki yako, ee Mtume wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23867/معنى-واتوب-الى-رسوله-في-الحديث
  • Imechapishwa: 23/05/2024