Msalimie unayemjua na usiyemjua

Swali: Tunaona kuwa watu wengi hawamsalimii mtu isipokuwa yule wanayemjua. Ni ipi nasaha yako?

Jibu: Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msalimie unayemjua na usiyemjua.”

Wasalimie Waislamu wote hata kama huwajui kwa kuwa ni Muislamu. Miongoni mwa haki za Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni kumsalimia pindi unapokutana naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015