Swali: Ni kipi kinachomlazimu yule mwenye kumuona mfungaji anayekula kwa kusahau?
Jibu: Amkumbushe. Kufanya hivo ni kusaidiana katika wema na uchaji Allaah. Ni kama ambavo mtu akimuona mwengine anaswali kuelekea kusikokuwa Qiblah, akamuona mtu anataka kutawadha kwa maji ya najisi na mfano wa hayo; basi ni lazima kumzindua mtu huyo. Ingawa mfungaji ni mwenye kupewa udhuru kwa kusahau kwake, lakini nduguye ambaye anaijua hali yake si mwenye kupewa udhuru. Kwa msemo mwingine ni lazima kwake kumkumbusha. Pengine hali hii inaweza kujengewa dalili kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika mimi si venginevyo ni mtu kama nyinyi. Nasahau kama nyinyi mnavosahau. Hivyo basi nikisahau, nikumbusheni.”[1]
Ikiwa yule mswaliji anatakiwa kukumbushwa, basi vivyo hivyo mfungaji pia anatakiwa kukumbushwa.
[1] al-Bukhaariy (401) na Muslim (572).
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/274)
- Imechapishwa: 03/05/2021
Swali: Ni kipi kinachomlazimu yule mwenye kumuona mfungaji anayekula kwa kusahau?
Jibu: Amkumbushe. Kufanya hivo ni kusaidiana katika wema na uchaji Allaah. Ni kama ambavo mtu akimuona mwengine anaswali kuelekea kusikokuwa Qiblah, akamuona mtu anataka kutawadha kwa maji ya najisi na mfano wa hayo; basi ni lazima kumzindua mtu huyo. Ingawa mfungaji ni mwenye kupewa udhuru kwa kusahau kwake, lakini nduguye ambaye anaijua hali yake si mwenye kupewa udhuru. Kwa msemo mwingine ni lazima kwake kumkumbusha. Pengine hali hii inaweza kujengewa dalili kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika mimi si venginevyo ni mtu kama nyinyi. Nasahau kama nyinyi mnavosahau. Hivyo basi nikisahau, nikumbusheni.”[1]
Ikiwa yule mswaliji anatakiwa kukumbushwa, basi vivyo hivyo mfungaji pia anatakiwa kukumbushwa.
[1] al-Bukhaariy (401) na Muslim (572).
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/274)
Imechapishwa: 03/05/2021
https://firqatunnajia.com/msahaulifu-anatakiwa-kukumbushwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)