Msahafu wa waqf hautolewi nje ya msikiti

Swali: Je, inajuzu kuchukua msahafu kutoka msikitini ulioandikwa juu yake “Waqf kwa ajili ya Allaah (Ta´ala)” ili kusomea nyumbani?

Jibu: Msahafu kama huo hauchukuliwi. Vitu vilivyowekwa waqf kwa ajili ya msikiti” vinabaki kwa ajili ya msikiti. Misahafu ya msikiti ibaki ndani ya msikiti. Aisome humohumo msikitini na asiitoe kutoka msikitini.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31390/ما-حكم-اخذ-مصحف-المسجد-للتلاوة-في-البيت
  • Imechapishwa: 24/10/2025