Matishio makali kwa anayeacha swalah ya ijumaa kusudi

Swali: Ni nini makusudio ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kuacha ijumaa mara tatu kwa uzembe, basi Allaah atampiga muhuri juu ya moyo wake”?

Je, anayechelewa mpaka imamu anamaliza Khutbah anaingia katika matishio haya?

Jibu: Onyo hili ni kwa yule ambaye amekosa swalah ya ijumaa mara tatu bila udhuru wowote. Atapigwa muhuri juu ya moyo wake. Ni onyo kali sana. Katika Hadiyth nyingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Watu wakome kuacha ijumaa. Vinginevyo Allaah atapiga muhuri juu ya mioyo yao, kisha watakuwa miongoni mwa wenye kughafilika.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Imekuja pia katika Hadiyth:

“Mwenye kuacha ijumaa tatu bila udhuru, atapigwa muhuri juu ya moyo wake.”

Haya ni matishio makali.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31391/ما-معنى-الوعيد-في-ترك-الجمعة-ثلاث-مرات-تهاونا
  • Imechapishwa: 24/10/2025