Swali: Mtu ni msafiri na amebakisha nusu saa au theluthi saa tu kuingia mjini kabla ya adhaana ya swalah. Je, anajuzu kwake kukusanya Maghrib na ‘Ishaa?
Jibu: Ndiyo, inajuzu kwake kukusanya Maghrib na ‘Ishaa, pia Dhuhr na Aswr, ikiwa muda wa Dhuhr au Maghrib umeingia na akaswali njiani, hapana vibaya. Hii ni kwa sababu anaweza kushughulishwa akishaingia mjini, pengine atakuwa amechoka au atabanwa na kazi. Akiamua kuswali pamoja na watu msikitini, basi hiyo itazingatiwa ni swalah ya kjitolea.
Swali: Aswali kabla hajawafikia au baada ya kuwafikia?
Jibu: Yeye ni msafiri. Kwa hiyo inafaa kwake kujumuisha Dhuhr na ‘Aswr, Maghrib na ‘Ishaa njiani, hata kama ataingia mjini kabla ya ‘Aswr au kabla ya ‘Ishaa.
Swali: Aswali ndani ya mji?
Jibu: Aswali njiani. Akishaingia mjini basi akaswali pamoja na watu, basi hiyo kwake itakuwa ni swalah ya kujitolea. Asiposwali hapana vibaya juu yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28543/هل-للمسافر-الجمع-قبل-نصف-ساعة-من-البلد
- Imechapishwa: 21/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)