Msafiri kukusanya swalah ingawa anajua atafika wakati wa swalah ya pili

Swali: Ikiwa mtu anataka kurudi katika mji wake na anajua atafika wakati wa swalah ya ´Ishaa – je, akusanye Maghrib na ´Ishaa au aswali Maghrib peke yake?

Jibu: Inaruhusiwa kukusanya njiani, kwa sababu huenda atakapofika atakuwa na mashughuli au anahitaji kupumzika. Hivyo inajuzu akusanya njiani, hata kama anatarajia kufika wakati wa ´Ishaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28897/حكم-الجمع-لمسافر-يصل-في-وقت-الثانية
  • Imechapishwa: 07/05/2025