Swali: Je, msafiri anapata dhambi akiswali kwa kukamilisha Rak´ah zote akiwa safarini au akifunga akiwa safarini bila kupata mashaka?

Jibu: Hapana, hana dhambi. Ana khiyari. Lakini kuacha kufunga ndio bora zaidi, na kuswali kwa kufupisha ndio bora zaidi.

Swali: Je, kuswali kwa kufupisha si jambo la lazima?

Jibu: Si la lazima, hapana. Lakini ni Sunnah. Hivyo akiswali kwa kukamilisha swalah yake, swalah yake ni sahihi, kama vile ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alivyokamilisha akiwa na Maswahabah katika hijjah nyingi na kama alivyokamilisha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31499/هل-ياثم-المسافر-اذا-اتم-او-صام-في-السفر
  • Imechapishwa: 25/10/2025