Msafiri aliye pekee anayeacha kuswali na msikitini

Swali: Je, msafiri analazimika kuswali kwa mkusanyiko?

Jibu: Ndiyo, akipata swalah ya mkusanyiko basi inamlazimu.

Swali: Vipi ikiwa kwa mfano anakaa hotelini?

Jibu: Aswali pamoja na mkusanyiko, hapaswi kuswali peke yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuswali kwa mkusanyiko. Aidha kuiacha ni miongoni mwa sifa za wanafiki. Lakini kama wako watu wawili au zaidi, basi wanaruhusiwa kuswali na mkusanyiko Rak´ah nne kama ambavo wanaruhusiwa kuswali wao wenyewe kwa kufupisha Rak´ah nne.

Swali: Je, mtu akiswali peke yake atapata dhambi?

Jibu: Ndiyo, kwa sababu swalah ya mkusanyiko ni wajibu.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28544/هل-تجب-الجماعة-في-الصلاة-على-المسافر
  • Imechapishwa: 22/04/2025