Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa ambaye hatendei kazi Hadiyth zilizosimuliwa na mpokezi mmoja katika ´Aqiydah?
Jibu: Hukumu yake ni kwamba ni mpotofu na mwenye kupotosha wengine. Hiyo ndio ´Aqiydah ya Mu´tazilah. Wanazuoni wamezungumzia jambo hilo. Imaam ash-Shaafi´iy ameyazungumzia katika “ar-Risaalah”, Imaam al-Bukhaariy katika “Kitab-ul-Aahaad” katika “as-Swahiyh” yake na Ibn-ul-Qayyim katika “Swawaa´iq-ul-Mursalah”. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا
”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”[1]
مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ
“Atakayemtii Mtume basi amemtii Allaah.”[2]
Mara nyingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akituma mjumbe mmoja. Bali Allaah (´Azza wa Jall) alimtuma Mtume akiwa peke yake. Wanazuoni wametafiti jambo hili. Wale wanaolingania kurudisha nyuma Hadiyth zilizopokelewa na mpokezi mmoja wanaita katika kuisambaratisha Shari´ah ya Allaah, kwa sababu sehemu kubwa ya Sunnah ni Hadiyth zilizopokelewa na mpokezi mmojammoja. Hiyo ni propaganda ya Mu´tazilah au ya kikafiri.
[1] 59:07
[2] 04:80
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 357-358
- Imechapishwa: 05/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket