Swali: Niliomba posa ya binti wa ami yangu rasmi. Nao uchumba kwetu huchukua muda mrefu, kama mnavyojua. Nikasafiri, kisha nikamuomba baada ya kusafiri anitumie picha yake, jambo ambalo walilifanya. Je, nina dhambi katika hilo? Ni ipi kafara yake?

Jibu: Haijuzu kuomba kutumiwa picha. Ni lazima kwako kutubu kwa Allaah na hiyo ndiyo kafara. Utubu kwa Allaah tawbah ya kweli kwa kujuta juu ya ulichofanya na kuazimia kutojirudia tena. Vilevile uiachane picha. Hilo ndilo wajibu kwako. Haifai kwa mwanamke kukutumia picha wala haifai kwako mwanaume kumtumia picha. Hata hivyo hapana vibaya kumwangalia iwapo umemposa au unataka kumposa. Hakuna tatizo ukamwangalia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha jambo hilo watazamane.

Kwa kifupi ni kwamba kumwangalia mchumba hakuna tatizo bila kuwa faraghani naye. Bali awepo babake, mamake au ndugu yake wa kiume bila kuwa faraghani naye. Aangalie uso wake na kilicho dhahiri kwake kama mikono yake au nywele zake. Hapana vibaya kufanya hivo. Lakini si haki yake kuwa faraghani naye wala kutoka naye kwenye gari, kama wafanyavyo baadhi ya watu pamoja na wachumba wao wakizunguka mjini au bustanini. Hayo ni maovu na ni njia ya ufisadi. Bali atamwangalia kwa kuwepo mlezi wake, mama yake au ndugu yake wa kiume na mfano wa hao ili aangalie kwake kile kitakachomvutia kwake au kitakachomfanya aache. Lakini haifai kwa mwanaume kuchukua picha yake, wala haifai kwa mwanamke kuomba picha yake. Vyote viwili ni vitu vilivyokatazwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7955/طلب-الخطيب-من-مخطوبته-صورة-لها
  • Imechapishwa: 06/09/2025