Mpangilio katika kuwapa zakaah wastahiki

Swali: Je, wanaopewa zakaah inakuwa kwa mpangilio kwa njia ya kwamba wanapangwa kama ilivyokuja katika Aayah?

Jibu: Sio kwa mpangilio. Bali pengine akapewa masikini na asipewe fakiri. Lakini kama inavyojulikana, yule ambaye ana haja zaidi ndio aula zaidi kupewa. Udugu na kuwa na haja zaidi vikikutana na ndugu huyu akawa sio miongoni mwa wale ambao wewe unawajibika kuwahudumia, anakuwa ni aula zaidi kuliko mtu wa mbali. Kadhalika mafukara wa nchini ni aula zaidi kuliko mafukara wa nje ya nchi yake. Vilevile yule ambaye yuko karibu na nchi yako ni aula zaidi kuliko alie mbali.

Check Also

Zakaah mke kumpa mume

Swali: Inajuzu kwangu kupokea zakaah ya dhahabu kutoka kwa mke wangu pamoja na kuzingatia kwamba …