Itambulike kuwa nasaha ni kumzungumzisha mtu kwa siri kati yako wewe na yeye. Ukimnasihi ilihali mko nyinyi wawili tu utamuathiri kwenye nafsi yake na atajua kuwa wewe ni mnasihiaji. Lakini ukimzungumza vibaya mbele ya watu anaweza kuingiwa na hasira na hivyo asikubali nasaha. Vilevile anaweza kufikiria kuwa malengo yako unataka kumlipiza, kumkabili na kuangusha hadhi yake mbele ya watu. Matokeo yake asikubali. Lakini ikiwa utafanya hivo kwa siri baina yako wewe na yeye, tendo hili litakuwa na mizani mizito kwake na maana. Matokeo yake akubali.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/398)
  • Imechapishwa: 29/07/2025